Arsenal wamethibitisha Sead Kolasinac atajiunga nao Mwezi Julai kama Mchezaji Huru na kwamba atasaini Mkataba wa muda mrefu baada ya kukamilisha taratibu zote za Uhamisho. Tangu Mwezi uliopita zilikuwepo habari kuwa Beki huyo wa Kushoto mwenye Miaka 23 atajiunga na Arsenal baada kumaliza Mkataba wake na Schalke ya Germany.
Inaaminika Everton, Manchester City na AC Milan zilitoa Ofa kumchukua Kolasinac, lakini mwenyewe ameamua kujiunga na Arsenal hasa baada kuthibitika Meneja Arsene Wenger atabakia Klabuni hapo baada kusaini Mkataba Mpya wa Miaka Miwili.
No comments:
Post a Comment