BUKOBA SPORTS

Sunday, June 4, 2017

RONALDO AMFUNIKA LIONEL MESSI UFUNGAJI BORA UEFA CHAMPIONS LIGI MSIMU HUU, APEWA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA FAINALI NA SIR ALEX!

http://a.espncdn.com/combiner/i?img=%2Fphoto%2F2016%2F0528%2Fr87341_1296x518_5%2D2.jpg&w=800&h=320&scale=crop&cquality=80&location=originCRISTIANO RONALDOCristiano Ronaldo makes history with CL final opener vs JuventusKABLA ya Fainali ya Jana ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, ambayo Mabingwa Real Madrid walitetea vyema Taji lao kwa kuifunga Juventus 4-1, Rekodi ya Cristiano Ronaldo ya Ufungaji Bora kwa Misimu Minne iliyopita ilikuwa hatarini.
Lionel Messi wa Barcelona ndie aliekuwa Juu akiongoza kwa Bao 1 huku Ronaldo akiwa na Bao 10.
Kabla Robo Fainali ya UCL Msimu huu Ronaldo alikuwa nyuma mno ya Messi akiwa na Bao 9 pungufu.

Cristiano Ronaldo makes history with CL final opener vs JuventusLakini Bao 5 katika Mechi 2 za Robo Fainali dhidi ya Bayern Munich zilimbeba na kwenye Nusu Fainali dhidi ya Atletico Madrid Ronaldo alipiga Hetitriki na kumfanya awe na Bao 10 dhidi ya 11 za Messi na yeye kutinga Fainali ya Jana huko Cardiff, Wales dhidi ya Juve akiwa na matumaini makubwa ya kumgalagaza Messi kwa Misimu Mitano ya Ulaya.
Jana, kwenye Fainali, Ronaldo alipiga Vao 2 Real ikiichapa Juve 4-1.
Cristiano Ronaldo makes history with CL final opener vs Juventus
Pia mara baada ya Fainali hiyo, Ronaldo alikabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Fainali hiyo kutoka kwa Sir Alex Ferguson ambae alikuwa na Ronaldo kwa Miaka 6 huko Man United.

UCL - WAFUNGAJI BORA:

12 Cristiano Ronaldo Real Madrid
11 Lionel Messi Barcelona
8 Edinson Cavani Paris
8 Robert Lewandowski Bayern
7 Pierre-Emerick Aubameyang Dortmund

Ronaldo pia ameikamata Rekodi ya Messi ya kupiga Hetitriki 7 kwenye UCL.
UCL - WAFUNGAJI BORA KWA MISIMU MFULULIZO:
5. Cristiano Ronaldo Real Madrid 2012/13, 2013/14, 2014/15, 2015/16, 2016/17
4. Lionel Messi Barcelona 2008/09, 2009/10, 2010/11, 2011/12
3. Gerd Müller Bayern 1972/73, 1973/74, 1974/75
3. Jean Pierre Papin Marseille, Milan 1989/90, 1990/91, 1991/92

No comments:

Post a Comment