Mapema Wiki hii, Wenger alisaini Mkataba Mpya wa kubakia Arsenal kama Meneja wa Miaka Miwili na hilo limechangia na kuhusishwa na kusaini Wachezaji Wapya
Mwenyewe Wenger amekiri kumtaka Winga wa Leicester City Riyad Mahrez.
Akihojiwa na TV ya beIN SPORT, Wenger amesema hatasaini zaidi ya Wachezaji Watatu.
Ameeleza: “Nasema Watatu hivi!”
Pia Wenger alifafanua kuwa Mastaa wake Mesut Ozil na Alexis Sanchez hataondoka Arsenal licha kuhusishwa na kuhama katika kipindi hiki.
Lakini Wenger amesisitiza kuwa Wachezaji hao watabaki Klabuni hapo na mazungumzo yataendelea kuhusu Mikataba yao Mipya.
No comments:
Post a Comment