Jose Mourinho ameonyesha umahiri wake wa kuwa kipa baada ya kushiriki mechi ya kuchangisha fedha kuwasaidia watu walioathiriwa na moto wa jengo la Grenfell.
Meneja huyo wa Manchester United alicheza kama kipa katika mechi hiyo Game4Grenfell kati ya timu mbili za watu mashuhuri na wacheza soka wa zamani.
Kikosi chake kilishindwa kwa mabao 5-3 kwa njia ya penalti, ambapo bingwa wa olimpiki Sir Mo Farah alifunga bao.
Takriban watu 80 walifariki wakati jengo la Grenfell lilishika moto magharibi mwa London tarehe 14 mwezi Juni.
Watu mashuhuri walishiriki mechi hiyo wakiwemo mcheza filamu Damian Lewis na Olly Murs.
Fedha kutoka kwa tiketi za mechi hiyo zilienda kwa mfuko wa wale walioathiriwa na janga la moto.
Wakati wa mapumziko waimbaji Rita Ora, Emeli Sande na Marcus Mumford walitumbuiza umati kwa nyimbo zao.
MATCH FACTS
Team Ferdinand:
First half: Seaman, Gabbidon, Hill, Shephard, Wilson, Farah, Lewis, Spoony, Murs, Crouch, Mumford
Second half: Given, Glen, Bircham, Hill, Impey, Wretch 32, Merson, Wood, Duff, Pizzorno, Tempah
Goalscorers: Farah 2, Edwards 75
Team Shearer:
First half: James, Little, Walker, Jones, Mack, Campbell, Redknapp, Dornan, Sinclair, Sutton, Cohen
Second half: James (Mourinho), Little, Walker, Bay, Smith, Sinton (Cocker), Jones, Morris, Sinclair, Bullion, Badillo
Goalscorers: Sinclair 14, 49
Booked: Sinclair, Mourinho
Referee: Mark Halsey
A minute's silence was held ahead of kick-off in memory of those who lost their lives in the Grenfell fire in June
McFly singer and guitarist Danny Jones challenges for the ball against Mo Farah during Saturday's game
No comments:
Post a Comment