Simba imezidi kujichimbia kileleni baada ya kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba hii leo jioni.
Bao za Simba Sc leo hii zimefungwa kipindi cha pili baada ya kumaliza dakika 45 timu zote mbili zikiwa 0-0. Bao la kwanza limefungwa na Said Ndemla na bao la pili limefungwa na John Bocco baada ya mabeki wa Kagera Sugar kujichanganya.
Kipindi cha pili dakika ya 70 Said Ndemla aliipatia Simba goli la Kwanza na kufanya Simba kuongoza kwa bao 1-0. Wakati huo baaada ya bao hilo Shomari Kapombe aliingia kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe Simba akichukua namba ya Gyan.
Kipindi hicho cha pili dakika ya 80 John Bocco aliipachikia Simba bao la pili Baada ya kazi nzuri ya Shomari Kapombe aliyeingia kipindi hicho cha pili na Simba kuwatandika bao la pili na Simba kuongoza bao 2-0' Hadi dakika 90 zinamalizika Simba 2-0 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Ushindi huo unawarudisha Simba kileleni wakiwa na pointi 32.
Kiungo wa Simba Hamis Said Juma (Ndemla) akipeta baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya timu ya Kagera Sugar. Picha zote na Faustine Ruta
Beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso akikimbiza mpira akiwa sambamba na mshambuliaji wa Kagera Sugar Emmanuel Okwi.
Kadi ya Njano ilitolewa kwa mchezaji wa Kagera Sugar Fakhi
Emmanuel Okwi akiwa Chini chaliii!!
Mshambuliaji wa Kagera Sugar akimwangalia Mwamuzi juu ya rafu aliyotendewa na Mchezaji wa Kagera Sukari.
Okwi akiwa chini
Mlinzi wa Kagera Sugar Asante Kwasi akijutia kukosa nafasi ya kufunga bao
John Bocco akiwa chini na mwezake wa Kagera Sugar baada ya patashika kutokea...kipindi cha pili. Picha zote na Faustine Ruta
Jukwaa kuu wakiutaza mchezo
Viongozi mbalimbali wakiwa jukwaa kuu wakiutaza mchezo Kagera sugar dhidi ya Timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam.

Hakuna kupita!! hapa!

Mchezaji wa Kagera Sugar alimdhibiti mchezaji wa Simba kupita hapa!
Kichuya akijiandaa kupiga kona.
Mavugo wakati huo akipiga jalamba
Patashika kwenye lango la Kagera Sugar kipindi cha pili
Juma Kaseja akimcheki John Bocco
John Bocco akimtoka Mohamed Fakhi wa kagera Sugar
Baada ya kumtoka aliachia pasi kwa Mdemla aliyemalizia nyavuni na kuwanyanyua mashabiki wa Simba kwenye Viti kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Shangwe kwa Ndemla
Wakipongezana kwa bao
Wachezaji wa Kagera Sugar baada ya mchezo kumalizika wakiwa wamepoteza mchezo huo wa bao 2-0 mbele ya timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment