
Manchester City imetinga fainali yao ya kwanza wakinolewa na Pep Guardiola wakati vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza ikiifunga Bristol City magoli 3-2 katika mchezo wa kombe la Carabao.
Ikiwa inaongoza kwa ushindi wa magoli 2-1 katika mchezo wa kwanza, magoli kutoka kwa Leroy Sane, Sergio Aguero na Kevin de Bruyne yaliihakikishia Manchester City kutinga fainali.

Aiden Flint akiifungia Bristol City goli la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 2-2

Kevin de Bruyne akiwa amefunga goli la tatu lililoipa ushindi Manchester City
No comments:
Post a Comment