Azam FC imeitoa Simba kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.
Simba walitua salama kwa ndege mjini Bukoba na walifanya mazoezi kwenye uwanja huo wa Kaitaba wakijiandaa kwa pambano hilo linalotarajia kuwa kali.
Wekundu hao wa Msimbazi wanashuka dimbani baada ya kuwachapa Singida United kwa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mganda Emmanuel Okwi baada ya juzi kutupia bao mbili peke yake wakati Simba ikiibuka na ushindi huo mnono, Ataendelea kutegemewa na timu yake kutokana na makali yake.
Na sasa Wekundu wa Msimbazi kwa kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi, wamewasili mapema Bukoba kwa usafiri wa anga ili kufanya maandalizi mazuri.
Kocha huyo tayari ametambulishwa rasmi, lakini haijaelezwa ameingia mkataba wa miaka mingapi.
Ilielezwa kuwa kocha huyo Mfaransa ametua Simba kwa ajili ya programu maalumu ya vijana na ile ya timu ya wakubwa.
Lechantre ambaye ataanza kazi timu itakaporejea kutoka Bukoba, aliomba apewe angalau miezi minne ili Simba wafurahie matunda yake.
No comments:
Post a Comment