BUKOBA SPORTS

Friday, February 23, 2018

ARSENAL YATINGA HATUA YA 16 BORA LICHA YA KUFUNGWA BAO 2-1

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema kikosi chake kinaridhika na matokeo ya kunusurika kutolewa na timu ya ndogo ya Ostersunds FK ya Sweden na kutinga hatua ya 16 bora katika Ligi ya Europa.
Arsenal waliokuwa wameshinda magoli 3-0 katika mchezo wa awali ilijikuta ikiduwazwa jana baada ya kutanguliwa kufungwa magoli 2, kabla ya kurejesha goli moja kupitia kwa Sead Kolasinac.
Wageni Ostersunds FK walipata magoli yao kupitia kwa Hosam Aiesh na Ken Sema hata hivyo Aresenal walijikuta wakinufaika na ushindi wa mchezo wa awali na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-2.
Hosam Aiesh akiachia shuti na kufunga mpira uliomshinda kipa David Ospina
Beki Sead Kolasinac akiachia shuti akifunga goli pekee la Arsenal

No comments:

Post a Comment