Liverpool imejiweka vyema katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata matokeo mazuri kwa robo fainali kwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Manchester City yaliyopatikana ndani ya dakika 31 za kwanza katika dimba la Anfield.Manchester City iliyofungwa mchezo mmoja katika Ligi Kuu ya Uingereza kwa magoli 4-3 Januari katika dimba la Anfield, ilijikuta ikiadhibiwa tena na Liverpool safari hii katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mohamed Salah alikuwa wa kwanza kufunga goli baada ya dakika 12 na kisha baadaye Alex Oxlade-Chamberlain akaongeza la pili dakika nane baadaye akiachia shuti kali la umbali 20 lililompita Ederson na Sadio Mane kufunga goli la tatu.
Mshambuliaji nyota wa Liverpool aliyekatika ubora wa hali ya juu Mohamed Salah akifunga goli
Nyota wa Senegal Sadio Mane akiifungia kwa mpira wa kichwa Liverpool goli la tatu
No comments:
Post a Comment