Luis Suarez amefunga goli lake la kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupita karibu mwaka mmoja wakati Barcelona ikiifunga Roma magoli 4-1 katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali.
Katika mchezo huo pia Barcelona ilinufaika na magoli mawili ya kujifunga la kwanza kutoka kwa Daniele de Rossi aliyekuwa akijaribu kuzuia shambulizi la Lionel Messi na la pili Kostas Manolas akajifunga.
Haukuwa usiku wa bahati kwa mshambuliaji nyota Lionel Messi, hata hivyo Barcelona ilifanikiwa kupata goli la tatu kupitia kwa Gerard Pique, huku Roma wakipata goli pekee kupitia kwa Edin Dzeko.
Gerard Pique akiangalia mpira alioupiga ukitinga wavuni na kuandika goli la tatu
Edin Dzeko akiufuata mpira wavuni baada ya kufunga goli pekee la Roma
No comments:
Post a Comment