BUKOBA SPORTS

Friday, March 30, 2012

JOHN BOCCO AASTAFU KUICHEZEA TAIFA STARS.


Maji yamemfika shingoni mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Azam, John Bocco 'Adebayor'.
Baada ya kuendelea kuzomewa mfululizo na mashabiki wa soka wakati akiwa anaichezea timu ya taifa, John Bocco leo ameamua kustaafu kuitumikia timu ya taifa ili kuepukana na shida anazozipata kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo ya taifa.


Bocco ndio amekuwa mchezaji anayezomewa mno wakati anapoichezea timu ya taifa, jambo ambalo limekuwa likimkosesha raha na amani kwa muda mrefu anapokuwa akiitumikia timu ya taifa lake.

"Nimefikia maamuzi haya baada ya kufikiria sana, nimekuwa nikijitoa kwa hali na mali kulitumikia taifa langu lakini mashabiki wa timu yetu wanaona sifai, hivyo ni bora nijitoe au nistaafu kuichezea timu hiyo ili kuepekana na dhahama zao. Naitakia kila kheri timu yangu ya taifa naipenda na nitaendelea kuipenda siku zote." - Alimaliza John Bocco ambae pia ameomba viongozi kuikemea tabia ya kuzomea zomea ovyo.

No comments:

Post a Comment