BUKOBA SPORTS

Saturday, March 31, 2012

YANGA NA SIMBA ZASAKA POINT VPL


YANGA-SSC-STRIPRATIBA:
Jumamosi Machi 31
Coastal Union v Yanga
Simba v African Lyon
Msimamo Timu za juu:


[Mechi walizocheza kwenye mabano]
1 Simba [21] Pointi 47
2 Azam [21] 44
2 Yanga [20] 43
4 Mtibwa [21] 34




TAARIFA:
Wakongwe Nchini, Yanga na Simba, ambao pamoja na Azam FC na pengine, kimahesabu tu, Mtibwa Sugar, ndio waliobaki kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom, Jumamosi Machi 31 wapo Uwanjani kusaka pointi muhimu.
Huku mechi zikizidi kuyoyoma kwa Wakongwe hao wakiwa wamebakisha mechi 5 tu kumaliza Ligi, Mabingwa watetezi Yanga watakuwa huko Tanga Uwanja wa Mkwakwani kucheza na Coastal Union na Jijini Dar es Salaam Uwanja wa Taifa vinara wa Ligi Simba watacheza na African Lyon.

Kwenye mechi ya Coastal Union na Yanga Mwamuzi ni Rashid Msangi wa Dodoma ambaye atasaidiwa na Rashid Lwena (Ruvuma) na Issa Malimali (Ruvuma).
Nae Mwamuzi Amon Paul wa Musoma ndiye atakayechezesha mechi ya African Lyon na Simba Uwanja wa Taifa na Viingilio kwenye mechi hiyo ni Sh. 3,000 kwa viti vya kijani na bluu, Sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, Sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP A ni Sh. 15,000.

No comments:

Post a Comment