BUKOBA SPORTS

Monday, April 9, 2012

ARSENAL YAITUNGUA MANCHESTER CITY, MAN U WAZIDI KUCHEKA "POINTI 8 MBELE"

Super strike: Arteta scores the winning goal
                           Mkwaju wa mbali wa Arteta umeipa ushindi Arsenal

Mkwaju wa mbali wa Mikel Arteta umeipa Arsenal ushindi muhimu na kuiacha Manchester City ikiwa pointi nane nyuma ya Manchester United katika ligi kuu ya England. 
 Out of control: Balotelli lunged in wildly on Alex Song
Yaya Toure alitoka mapema kutokana na kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na David Pizzaro huku Balotelli akitolewa kwa kadi nyekundu.
Mara mbili Robin Van Persie aligonga mwamba huku mkwaju mwingine aliopachika wavuni ukiwa wa kuotea.
 Getting in the way: Robin van Persie has an effort on goal that hits team-mate Thomas Vermaelen and goes over
Arteta alipata mwanya katika dakika ya 86 kwa kuachia mkwaju umbali wa yadi 25.
Jumping for joy: Arsenal fans do the Poznan celebration                                                  Mashabiki wa Arsenal wakishangilia

Arsenal walitawala kabisa Mechi hii na kukosa bao mbili za wazi na Man City walikuwa na wakati mbovu hasa yule ‘Toto Tundu’-‘Kwanini kila Siku mie’- Mario Balotelli akistahili kupewa Kadi Nyekundu mara 3 katika Kipindi cha Kwanza lakini akaambulia Kadi ya Njano na hatimaye kupata nyingine ya pili katika Dakika ya 89 na kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Battle for the ball: Vermaelen collides with Manchester City's Sergio Aguero
Bao la ushindi kwa Arsenal, bao tamu sana, lilifungwa Dakika ya 86 na Mikel Arteta kwa kigongo cha mbali.

Vikosi vilivyoanza:

Arsenal: Szczesny, Sagna, Koscielny, Vermaelen, Gibbs, Arteta, Song, Walcott, Rosicky, Benayoun, van Persie

Akiba: Fabianski, Andre Santos, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Djourou, Jenkinson, Chamakh.

Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Clichy, Toure Yaya, Barry, Milner, Aguero, Nasri, Balotelli

Akiba: Pantilimon, Richards, Pizarro, Dzeko, Kolarov, Tevez, De Jong.

Refa: Martin Atkinson





Arsenal sasa wamerejea katika nafasi ya tatu, pointi mbili juu ya Tottenham walio nafasi ya nne.
Time to go: Balotelli is sent off in the final minute
                Nimekuvumilia sana toka nje sasa.... Mario Balotelli akipewa kadi nyekunduAll over? The Manchester City players look dejected at the final whistleMwisho: Dakika 90 zikaisha Man city wakatoka kapa na huku wakiduwaa kama ligi imeisha.



[MECHI ZILIZOBAKI kwa Man United & Man City]
Man City
Man Utd
Jumatano Aprili 11
Man City v West Brom
Jumamosi Aprili 14
Norwich v Man City
Jumapili Aprili 22
Wolves v Man City
Jumatatu Aprili 30
Man City v Man Utd
Jumamosi Mei 5
Newcastle v  Man City
Jumapili Mei 13
Man City v QPR
Jumatano Aprili 11
Wigan v Man United
Jumapili Aprili 15
Man United v Aston Villa
Jumapili Aprili 22
Man United  v Everton
Jumatatu Aprili 30
Man City v Man United
Jumamosi Mei 5
Man United v Swansea
Jumapili Mei 13
Sunderland v Man United

No comments:

Post a Comment