Mabingwa watetezi Manchester United jana waliwaachia zigo kubwa Mahasimu wao Manchester City baada ya kuwachapa QPR bao 2-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na kujizatiti kileleni wakiwa Pointi 8 mbele na hivyo kuwafanya Man City, wanaocheza ugenini Emirates, Man city nao mambo hayakwenda saaafi baada ya kutunguliwa goli 1-0 na Arsenal. City wamelazimika kupoteza pointi tatu baada ya kukomaliwa na wazee wa mtutu Arsenal. Kutwaa Ubingwa City umeyeyuka huku Mechi za Msimu huu zikiendelea kuyoyoma wao wakiwa wamebakisha Mechi 6 na Man United Mechi 6.
Bao la kwanza lilifungwa na Wayne Rooney kwa penati ambayo imezua utata kwa madai kuwa Ashley Young, alipopasiwa mpira na Rooney, alikuwa ofsaidi na pia hakuchezewa rafu na Beki wa QPR Derry.
Tukio hili la Dakika ya 13 lilimfanya Derry apewe Kadi Nyekundu na Refa Lee Mason na Rooney kufunga penati hiyo.
Ashley Young akianguka chini eneo la hatari na kupewa Red kadi Shaun Derry
Shaun Derry aliyepewa kadi nyekundu akitoka uwanjani
Wayne Rooneyakipiga mkwaju wa penati, alifunga hiyo penati na ikawa 1-0 kipindi cha kwanza
Rooney: akifunga penati
QPR manager Mark Hughes hakufurahia kitendo cha refa kutoa penati na red kadi
Lakini katika Dakika ya 68 Mkongwe Paul Scholes alikata ngebe zote kwa shuti la Mita 25 lililoambaa na kudunda chini mbele ya Kipa Kenny aliedaivu na kwenda moja kwa moja ndani ya kamba na kuandika bao la pili.
Brothers in arms: Manchester United's Rio Ferdinand shakes hands with brother Anton
MSIMAMOTIMU ZA JUU
[Kila Timu imecheza Mechi 32 isipokuwa inapotajwa]
1 Man United Mechi 32 Pointi 79
2 Man City Mechi 32 Point 71
3 Tottenham Mechi 32 Pointi 59
4 ArsenalMechi 32 Point 61
Mechi inayofuata kwa Man United ni Jumatano watakapokuwa wageni wa Wigan.
Vikosi vilivyoanza:
Man United: De Gea; Rafael, Ferdinand, Evans, Evra; Valencia, Carrick, Scholes, Young; Rooney, Welbeck.
Akiba: Amos, Jones, Giggs, Park, Hernandez, Cleverley, Pogba.
QPR: Kenny, Onuoha, Ferdinand, Hill, Taiwo, Diakite, Derry, Mackie, Taarabt, Buzsaky, Bothroyd
Akiba: Cerny, Gabbidon, Campbell, Young, Smith, Wright-Phillips, Zamora.
Refa: Lee Mason.
No comments:
Post a Comment