BUKOBA SPORTS

Monday, April 9, 2012

RATIBA YA MAZISHI YA KANUMBA:KUZIKWA JUMANNE(KESHO) KINONDONI JIJINI DAR-ES-SALAAM

 
TAARIFA YA KUMUAGA NA MAZIKO YA STEVEN KANUMBA 09/04/2012
 
 
Kesho, Jumanne tarehe 10 Aprili 2012 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tisa alasiri, mwili wa marehemu Steven Charles Kanumba utakuwa katika viwanja vya Leaders (Leaders Club) kwa ajili ya kuagwa.

Baada ya kuagwa, mwili wa marehemu utaelekea kwenye makaburi ya Kinondoni ambapo shughuli za maziko zitaana saa 10 alasiri kwa ajili ya kupumzishwa.



Mama mzazi wa Steven Kanumba anayeitwa Flora Mtegoa (katikati aliyeshika tama), akiwa amezungukwa na ndugu,jamaa na waombolezaji wengine mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sinza-Vatican




Hivyo Kanumba atazikwa makaburi ya kinondoni na ataagwa siku ya jumanne katika viwanja vya leaders kinondoni.

PICHA YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumba alizaliwa Januari 8, mwaka 1984, mkoani Shinyanga, kabla ya umauti kumfika Aprili 6, mwaka 2012.
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, Shinyanga na baadaye akajiunga na sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Ni wakati huo akiwa Jitegemee, Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania kuna filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa na hii sehemu ya kazi nzuri ya Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood, Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin. 
 


MKE WA WA WAZIRI MKUU PINDA AKIWEKA SAINI KWENYE KITABU CHA MAOMBOLEZO CHA MSANII MAARUFU STEVEN KANUMBA
WAZIRI WA USHIRIKIANO AFRICA MASHARIKI MH: SAMWELI SITA NAYE ALIWEKA SAINI

RIDHIWAN KIKWETE NAYE ALIWEKA SAINI KWENYE KITABU CHA MAOMBOLEZO 

No comments:

Post a Comment