BUKOBA SPORTS

Monday, April 9, 2012

REBECCA MALOPE ATIKISA WATU UWANJA WA TAIFA TAMASHA LA PASAKA

Mwimbaji wa muziki wa injili Rebecca Malope kutoka nchini Africa Kusini akiimba huku akisindikizwa na gwiji wa nyimbo za injili Rose Muhando  wa pili kutoka kushoto mara baada ya kufanya onyesho la kukata na shoka kwenye tamasha la muziki la Pasaka jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, wanamuziki wengi wa kimataifa wametumbuiza katika tamasha hilo wakiwemo Solomon Mukubwa mkutoka Congo DRC, Joshua Sekereti kutoka Zambia, Emi Kosgei kutoka Kenya na  Anastazia Mukabwa kutoka Kenya, hapa nyumbani walikuwepo Rose Muhando mwenyewe, Christine Shusho na wengine

 Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchini Afrika Kusini Rebecca Malope akiimba katika tamasha la pasaka linalofanyika kwenye uwanja wa taifa usiku huu, tamasha hilo limeanza tangu mchana na waimbaji wengi wameshaimba na kutoa burudani ya kutosha kwenye uwanja wa Taifa
 Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchini Afrika Kusini Rebecca Malope akicheza huku Msanii wa muziki Dokii akicheza naye katika tamasha la muziki la Pasaka kwenye uwanja wa Taifa.
 Mwimbaji Rose Muhando akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wa Taifa usiku huu.
 Rose Muhando akiimba na kucheza na kundi lake jukwaani.
Rose Muhando akiimbisha mashabiki kwenye uwanja wa taifa ambao wameonekana kuchanganyikiwa sana na nyimbo zake hasa wimbo wa "Utamu wa Yesu"

No comments:

Post a Comment