BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 11, 2012

BARCELONA WAIFUKUZIA KWA KASI REAL MADRID YAICHAKAZA GETAFE 4-0, LIONEL MESSI AFUNGA LA 61

                              Messi anavyotupia kitu kwenye nyavu

Lionel Messi amefunga bao la 61 usiku wa kuamkia leo na kutoa pasi mbili za mabao, akiiongoza Barcelona kuichapa Getafe 4-0 katika La Liga na kuwafanya mabingwa hao watetezi sasa wazidiwe pointi moja tu na vinara wa Ligi ya Hispania, Real Madrid.
Messi aligongeana vizuri mno na Andres Iniesta kabla ya kufunga dakika ya 44. Messi sasa anaongoza kufunga mabao katika La Liga akiwa ana mabao 39, bado moja tu kufikia rekodi aliyoweka Cristiano Ronaldo msimu uliopita. 


Lionel Messi celebrates after doubling Barcelona's lead against Getafe

Messi amefunga mabao 12 katika mechi zake 13 zilizopita, akifanya jumla ya mabao 24.
Ni mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 60 katika ligi kubwa za Ulaya, tangu mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich, Gerd Mueller alipofikisha mabao 67 msimu wa 1972-73.
Alexis Sanchez alifunga dakika ya 13 na 73 na Pedro Rodriguez akafunga dakika ya 75, wakiiwezesha Barcelona kushinda mechi ya 10 mfululizo ya ligi.
Real Madrid inaweza kurejesha pengo la pointi nne dhidi ya Barca, iwapo itashinda mechi yake ya leo dhidi ya Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment