BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 4, 2012

GARETH BALE - NILIKATAA KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED NIKAJIUNGA NA SPURS


Gareth Bale amefichua siri kwamba alikataa kujiunga na Manchester United kabla ya kuchagua kwenda Spurs.

Winga huyo wa kimataifa wa Wales alipewa ofa ya kuhamia Old Trafford na Boss United Sir Alex Ferguson alipokuwa na miaka 17 akiichezea Southampton.


Lakini kinda hilo alichagua kwenda Tottenham baada ya kuhakikishiwa nafasi katika kikosi cha kwanza, hivyo akaamua kumtosa Fergie.


Bale, 22, alisema: "Man United walikuwa wakinitaka lakini mimi nilikuwa nataka nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Hivyo niliona mahala pa ukweli ambapo ningepata nafasi hiyo ni Spurs.


"Kocha wa kipindi kile Martin Jol aliniambia alikuwa akitaka niingie moja kwa moja katika kikosi cha kwanza, na hicho ndicho kilichonivutia zaidi."


Bale pia amefichua alikuwa na nafasi ya kuichezea England lakini akaamua kuichezea Wales.

No comments:

Post a Comment