BUKOBA SPORTS

Saturday, April 7, 2012

NEWCASTLE UNITED YAIKANDAMIZA SWANSEA CITY 2-0

Newcastle United imezidi kujiongezea matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaysa msimu ujao, baada ya kuichapa mabao 2-0 Swansea City, shukrani wake Papiss Cisse aliyefunga mabao hayo yote.

Mshambuliaji huyo Senegal aliye kwenye ‘fomu’ ya juu aliwafungia bao la kwanza The Magpies mapema tu baada ya kuikimbilia pasi ya Yohan Cabaye na kumtungua kipa wa Swans, Michel Vorm akiwa umbali wa yadi 20.

Swansea ‘Barca ya England’ ilitawala mchezo, lakini Newcastle ilicheza kwa mipango zaidi na kufanikiwa kupata walichokuwa wakihitaji.

Ushindi huo wa nne mfululizo kwa Newcastle

Newcastle unakihakikishia kikosi cha Alan Pardew kuipiku Chelsea katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikizidiwa pointi mbili tu Tottenham Hotspur na Arsenal, ambao wanakalia nafasi mbili za mwisho za kucheza Ligi ya Mabingwa.

Lakini Newcastle imejiwekea matumaini ya kurejea kwenye michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2006-2007, kikosi cha Pardew kikiwa katika kiwango kizuri zikiwa zimebaki mechi sita, wakati Cisse, ambaye sasa amefunga mabao tisa katika mechi nane tangu asajiliwe Januari.

No comments:

Post a Comment