BUKOBA SPORTS

Saturday, April 7, 2012

CHANZO CHA KIFO CHA KANUMBA CHA ELEZWA


Mdogo wake na marehemu Kanumba akiongea na waandishi wa habari

Mdogo wake  marehemu steve kanumba, Ameeleza  kuwa elizabeth michael  maarufu kama lulu alikuja nyumbani kukawa na kaugomvi ambapo wakaingia chummbani wakiwa huko baada ya muda,lulu alitoka na kumuita yeye  kumuambia kanumba kaanguka, ye alipoenda akamkuta kaanguka ndio akaenda muita daktari wa kanumba ambapo aliporudi hakumkuta lulu, lakini  hadi tunavyoongea lulu yuko polisi osterbay kwa ajili ya mahojiano na polisi.

 

ELIZABETH MICHAEL LULU
Imethibitishwa kuwa kifo chake kimetokea  usiku wa kuamkia leo. Bado kuna taarifa tata juu ya sababu ya kifo chake. Habari zaidi zitawajia kadri tutakavyozipokea.
 








Hii ndo nyuma aliyo kuwa akiishi kanumba

Umati wa watu warika zote waliofunga barabara walio fika kwenye msiba wa kanumba.

Picha iliyoko sebuleni kwa kanumba



Umati wa watu ukiwa katika hali ya sijitambui nje ya nyumba aliyokuwa akiishi msanii wa filamu za bongo nchini Steven Kanumba.



Mtangazaji wa East Africa Radio Anne Peter akifanya mahojiano na mmoja wa ndugu wa marehmu.

Mdogo wa marehemu Seti Bosco aliyekuwa akiishi na marehemu Steven Kanumba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusiana na kifo cha aliyekuwa msanii wa filamu za Kitanzania.
Kwa mujibu wa Bwana Bosco marehemu alikuwa na bifu na Elizabeth Michael a.k.a LULU mara ya mwisho alimwabia Seti nenda chumbani Kaka yako amezimia, na kwa mujibu wa taarifa alipokwenda chumbani inasemekana alimkuta amezimia huku akiwa anatokwa na povu mdomo.


Pichani Juu na Chini ni baadhi ya wasanii wa filamu nchini wakiwa hawaamini taarifa za kifo cha Steven Kanumba.


“Siamini kama amekufa”…Steve Nyerere akiongea na waandishi wa habari.

 Baadhi ya wasanii wakiomboleza kwa majonzi.

 ”Bwana ametoa na Bwana ametwaa”. Asha Baraka, Eric Shigongo na H. Baba nyumbani kwa marehemu.

 Ndugu, Jamaa na marafiki wakiendelea kuwasili.

Aliyewahi kutwaa taji la Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu katika huzuni.
Vilio na Simanzi vimetawala nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba.

Vitu vimetolewa ili watu waweze kukaa vizuri msibani

Jackline Wolper akiwa amezimia

Baadhi ya waombolezaji




                                        ile kumi alfajiri tayari wasanii karibia wote walishafika



                             watu ni wengiii mnooooo
                             vyombo vya habari karibia kila kona







Mwanamitindo Happiness Magesse alipofika kwenye msiba wa kanumba

Hii ndio nyumba aliyokuwa anaishi kanumba.

Hii ni sehemu ya umati uliofika nyumbani kwake.

Gari la polisi likiwa linaingia.

Hili ndio gari la polisi lililoleta askari kwa ajili ya uchunguzi.

No comments:

Post a Comment