BUKOBA SPORTS

Thursday, April 5, 2012

LAPF YAPIGA JEKI NGUMI ZA RIDHAA



MFUKO wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF) umetoa vifaa kwa timu ya taifa ya ndondi za ridhaa vyenye thamani ya Sh milioni 6 kwa ajili ya timu ya taifa inayojiandaa kwa mashindano ya kusaka nafasi ya kushiriki Michezo ya Olimpiki.

Timu ya taifa ya ndondi za ridhaa imepiga kambi katika shule ya sekondari ya Filbert Bayi iliyoko Kibaha mkoani Pwani, ikijiandaa na mashindano hayo ya mchujo yatakayofanyika Casablanca, Morocco kuanzia Aprili 27 hadi Mei 6 mwaka huu.


Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Idara ya Ushirika, Mawasiliano na Masoko, Andrew Kuyeyana alisema kuwa LAPF itaendelea kuisaidia timu hiyo, ili kuhakikisha mchezo wa ndondi unarudi katika heshima.


Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Henry Lihaya akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema kuwa, LAPF imetoa funzo kwa mifuko na taasisi zingine kuichangia timu hiyo ya taifa.

No comments:

Post a Comment