BUKOBA SPORTS

Thursday, April 12, 2012

MANCINI: HATUWEZI KUSHINDA LIGI

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini anasema timu yake haiwezi kuchukua ubingwa mwaka huu wa ligi kuu ya England licha ya kupunguza wigo wa pointi hadi tano kati yao na viongozi Manchester United.
City waliwafunga West Brom 4-0 siku ya Jumatano, huku Manchester United wakifungwa 1-0 na Wigan, na kufufua ndoto zao za kushinda ligi ikiwa imebaki mechi tano msimu kumalizika.
"Mambo kwisha sasa," alisema Mancini. "pointi tano ni nyingi sana.
"Manchester United wamejitahidi sana. Sisi hatuna moyo huo."
Katika tathmini ya mechi ya Jumatano - ambayo City ilipata ushindi mkubwa kutokana na magoli mawili kutoka kwa Sergio Aguero na mengine kutoka kwa Carlos Tevez na David Silva - Mancini alisema kuwa "kila kitu kinawezekana".
Meneja huyo raia wa Italia amekanusha kuwa anajaribu kucheza mchezo wa akili baada ya ushindi wao wa nyumbani katika uwanja wa Etihad na akaongeza atahakikisha kuwa timu yake inamaliza msimu vyema.

No comments:

Post a Comment