Pia asilimia mbili ya mapato yatakayopatikana kwenye mechi ya Twiga Stars na Bongo Movie yatakwenda kwenye familia ya mwigizaji nguli wa filamu Tanzania, Stephen Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7 mwaka huu.
Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh. 10,000 kwa VIP A, sh. 5,000 kwa VIP C na B na sh. 2,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu. Mechi itaanza saa 10 kamili jioni.
Twiga Stars itacheza mechi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Ethiopia jijini Addis Ababa. Mechi hiyo itachezwa Mei 26 mwaka huu na wiki mbili baadaye timu hizo zitarudiana jijini Dar es Salaam. Twiga Stars ilifuzu raundi hiyo baada ya kuitoa Namibia kwa jumla ya mabao 7-2.
Machi 10 mwaka huu, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alizindua akaunti ya Twiga Stars kupitia Tigo Pesa kuichangia timu hiyo ambayo inashiriki michuano ya AWC. Wachangiaji wanatakiwa kutuma mchango wao kwenda namba 13389.
No comments:
Post a Comment