Kanumba Enzi za uhai wake

PUMZIKA KWA AMANI STEVEN KANUMBA THE GREAT
Ni majonzi makubwa sana kwa Watanzania wote sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi, inauma sana kwa kijana mdogo kama Kanumba kufariki wakati alikuwa bado hajazitima ndoto zake .Mungu ailaze roho ya marehemu Swaiba wangu Steven Kanumba ni mengi sana tuliyoyafanya mimi na wewe katika gurudumu ili la sanaa bila kujali yote yaliyotokea ni kawaida ya binadamu kutoelewana kama Baba na Mama wanafunga ndoa kanisani na wanakula viapo vya utii mbele za Mungu lakini wanagombana na kufikia hatua ya kuachana kwanini ishindikane kwetu ni hali ya kwaida katika maisha binadamu kutofautiana mengi yanazungumzwa juu yangu ila kila kitu mimi namuachia Mungu mimi ni mnyonge siwezi kupambana nanyi mnaoniongelea vibaya maumivu nayoyapata juu yenu Mungu hatowaacha siwezi kuzizuia hisia zenu kuzungumza yale mnayojisikia.
Muda mfupi tu baada ya kufariki Steven Kanumba akiwa kwenye gari lake la kifahari Lexus tangulia ndugu yangu sisi tuko nyuma yako maana kila nafsi itaonja umauti. Wadau nilikuwa kimya kwa kutowaletea matukio kwa sababu ya shughuli zilkuwa nyingi sana katika msiba nilikuwa kwenye kamati ya mazishi hivyo sikuwa nikipata muda wa kutosha na sio watu wanavyofikiria jamani hata kama kuna matatizo ndio katika maswala ya msiba hapana jamani mimi sijafikia hali hiyo yakuwa na roho ya kinyama namna hiyo
Hapa tukiutelemsha mwili wa marehemu katika hospital ya Muhimbili ni mtu wa kwanza kufika katika eneo la tukio
Tukimfunika rafiki yetu katika safari yakuelekea mochwali
Safari yetu ya mwisho binadamu wote mara ya kwanza nilipofika walikataa kumpokea pale hospital mpaka wapate PF 3 ndipo nilipowasha gari na kwenda Salenda polisi na kuwapata askari watatu ndipo tukapata fursa ya kwenda kumpuzisha marehemu
Tukimfunika macho maana yalikuwa wazi kama anasinzia
Macho yakiwa yamefumba baada ya kumfumba
Msiba tukaupeleka nyumbani kwake Kanumba na umati mkubwa ulikuwepo ukiwa una majonzi makubwa kwa kumpoteza mpendwa wao
Viongozi mbalimbali wa serikali waliudhuria Mrema wa kati akiingia ni mbunge wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na alishawahi kuwa waziri wa mambo ya ndani
Waheshimiwa wakiteta jambo
Kitabu cha kumbukumbu na picha ya marehemu
Waziri wa ofisi ya Rais na mausiano Mueshimiwa Steven Wasira akindiaka ujumbe wake kwenye kitabu cha kumbukumbu
Waziri Mkuu Peter Kayanza Pinda akiwasili kwenye msibani kwakweli tunawashukuru sana serikali yetu kwa kuweza kutufariji katika kindi kigumu tulichokuwa nacho kwa sasa mmetutia moyo kwakweli
Mueshimiwa Zito wa kushoto mbunge wa Kigoma mjini naye alikuwepo tunakushukuru sana ndugu yetu
Waziri Mkuu akiongea na mwenyekiti wa kamati ya mazishi bwana Gabriel Mtitu aliyevalia nguo nyeusi
wakiendelea kuteta jambo
Rais wa nchi mueshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete naye akiwasili
Naye akifikia kwenye kitabu cha kumbukumbu
Mambo yakiendeleaa.....
Hapa akiongea jambo na baadhi ya wanakamati ya mazishi
Mwenyekiti wa Bongo Movie Jb akiteta jambo na Mueshimiwa Rais
Tunakushukura sana Rais wetu kwa kuja kutufariji
The Greatest nikimsikiliza Rais
Hapa akiondoka uku akiwasalimia Wananchi wake
Poleni sana hayo ni maneno yake Mueshimiwa Rais
Baada ya kuondoka Rais tukawa tunateta jambo ambalo lilimchekesha sana mtoto wa Rais Riz One Kkikwete
The Greatest nikiwa katika maojian na mwandishi wa habari
Mzee Chilo akiongea jambo na Steve Nyerere
Salama Jabir na Madam Ritha wakiwa kwenye majonzi
Dulla wa Planet Bongo na Salama Jabir
wadau |
Ruge akiwa na waheshimiwa |
Musa K akiwa amefika kufariji wafiwa |
Monalisa,Millen & Ruge |
No comments:
Post a Comment