BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 25, 2012

PEP GUARDIOLA AKILI NI LAZIMA KUBADILI AINA YA UCHEZAJI!

BASI LA BARCA LAKOSA ABIRIA, WAPIGIWA KWAO 
 
NINI WANAHABARI WANASEMA HUKO SPAIN

Meneja wa Barcelona, Pep Guardiola, amekiri kipigo walichokipata toka kwa Chelsea iliyowabwaga nje ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kuwachapa jumla ya bao 3-2 katika Mechi mbili kitailazimisha Timu yake ibadili mbinu ingawa alisisitiza Timu yake ilicheza vizuri mno.
 Pep Guardiola

Chelsea waliichapa Barcelona bao 1-0 katika Mechi ya kwanza na jana kutoka sare bao 2-2 Uwanjani Nou Camp huku wakicheza Mtu 10 kwa muda mrefu na kutinga Fainali hapo Mei 19 itakayochezwa Allianz Arena, Munich ambayo watakutana na Mshindi wa leo kati ya Real Madrid na Bayern Munich.
Akiongea baada ya Mechi, Guardiola alisema: ‘Nilileta mfumo huu ‘shambulia, shambulia, shambulia’ lakini sasa tumejifunza, inabidi tutafute njia nyingine ya kushambulia vizuri zaidi.’
Baadhi ya Wadau wamekuwa wakidai Barca imekuwa ikimtegemea sana Nyota wao Lionel Messi na Siku akifunikwa tu magoli hayapatikana na wengine wamesema sasa Barca inabidi wawakumbuke na kurudisha aina ya Mastraika halisi kama walivyokuwepo zamani kina Zlatan Ibrahimovic na Samuel Eto’o.

NINI WANAHABARI WANASEMA HUKO SPAIN:
GAZETI la Marca: "Usiku Mbaya wa Leo!" ‘Bahati mbaya siku zote huenda kwa yule anaestahili. Kama Messi, ambae amekuwa na Msimu mzuri, alivyogundua jana na pia Klabu imejiingiza kwenye jinamizi kubwa kupita yote enzi za Guardiola!’
•Sport: "Soka yaiadhibu Barca kwa kuibwaga kikatili!" – ‘Ni ngumu kueleza jinsi gani Timu inapoteza mechi ambayo walikuwa bora kupita Wapinzani wao. Chelsea iliyocheza Nou Camp ilikuwa kama ile iliyocheza Stamford Bridge-wabahili, waoga, wanakera!’
•AS: ‘Hadithi ya uhanithi!’ - ‘Ni ukatili na haikustahili lakini ni sahihi-Barca walikuwa bora, Chelsea walikuwa washindani wazuri!’

Spanish Paper ASAkiongea zaidi, Guardiola alisema: ‘Kitu cha kwanza kilichoingia akilini mwangu ni huzuni! Nilisima mbele ya Timu nikijiuliza nini tumekosea kwa kutofika Fainali lakini nilishindwa. Upinzani ulikuwepo, wakijihami sana lakini wazuri katika kaunta ataki! Tulifanya kila kitu lakini tulishindwa kufunga bao jingine na Soka ni magoli!’
Pia, Guardiola alisema kuwa ataamua kuhusu kuongeza Mkataba wake, unaomalizika mwishoni mwa Msimu huu, katika Siku chache zijazo.
Pigo la jana linafuatia kipigo cha 2-1 walichopewa Jumamosi na Real Madrid na hivyo kufuta matumaini ya kutetea Ubingwa wao wa La Liga na kuwaacha na Fainali ya Copa del Rey watakayocheza na Athletic Bilbao hapo Mei 20 kuwa ndio michuano pekee wanayoweza kutwaa Taji lingine.
Kwa kubwagwa na Chelsea, Barca walishindwa kuweka rekodi ya kuwa Timu pekee baada ya AC Milan ya Mwaka 1990 kuweza kutetea vyema Ubingwa wao wa Ulaya.

No comments:

Post a Comment