BUKOBA SPORTS

Thursday, April 26, 2012

UEFA CHAMPIONS LIGI: FINALI NI BAYERN MUNICH V CHELSEA MEI 19, 'REAL YALALA KWA MATUTA ' YAWAFATA BARCELONA!!

Down and out: Jose Mourinho was left dejected by Real Madrid's penalty shootout loss to Bayern Munich
kilicho wapata  Barca chawapata na Real Madrid.......
Bayern Munich watakutana na Chelsea kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kuwabwaga Real Madrid kwa mikwaju ya penati tano tano, Fainali ambayo itachezwa nyumbani kwa Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena ambao kwa siku hiyo tu, kwa sababu za kiudhamini, utaitwa Fußball Arena München.
 Hero to villain: Cristiano Ronaldo scored twice but had his penalty saved in the shootoutPENATI YA RONALDO ALIYOKOSA HII HAPA... ALICHOKA HOI JANA!
Dejected: RonaldoRonaldo Hoi baada ya kuikosa Penati
Real Madrid, waliokuwa nyuma kwa bao 2-1 baada ya kufungwa Mechi ya kwanza, walianza kwa moto sana pale walipokuwa mbele kwa bao mbili za Cristiano Ronaldo ndani ya Dakika 14, moja likiwa la penati, lakini, Arjen Robben, akasawazisha kwa penati katika Dakika ya 27 na kufanya ngoma iwe 2-1 na hivyo sawa kwa jumla ya bao 3-3 kwa Mechi mbili.
 Remember me? Arjen Robben (right) is one former Chelsea player heading for a reunion
Hadi Dakika 90 matokeo yalibaki hivyo hivyo na Dakika 30 za nyongeza hazikubadili kitu na ndipo ikaja tombola ya mikwau ya penati na Bayern Munich kuibuka kidedea kwa penati 3-1.
 Final countdown: Bayern celebrate after Bastian Schweinsteiger (centre) scored the winning penalty
Bastian Schweinsteiger ndie aliefunga penati ya mwisho lakini Kipa wa Bayern, Manuel Neuer, alikuwa Shujaa pia baada ya kuokoa penati za Ronaldo na Kaka.

Got the T-shirt: Mario Gomez (left) and Manuel Neuer (right) celebrate after the match
Got the T-shirt: Mario Gomez (left) and Manuel Neuer (right) Wakishangilia kwa furaha kubwa jana

MIKWAJU ya PENATI:
-David Alaba [Bayern]-afunga bao 1-0
-Ronaldo [Real]-iliokolewa 1-0
-Gomez [bayern]-afunga 2-0
-Kaka [Real]-iliokolewa 2-0
-Kroos [Bayern]-iliokolewa 2-0
-Alonso [Real]-afunga 2-1
-Lahm [Bayern]-iliokolewa 2-1
-Ramos [Real]-akosa 2-1
- Schweinsteiger [Bayern]-afunga 3-1

Agony: Madrid players react during their penalty shootout defeat at the Bernabeu
Hii ni mara ya pili kwa Cristiano Ronaldo kukosa penati katika Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwani alikosa moja kwenye mikwaju mitano mitano ya penati katika Fainali alipokuwa na Manchester United walipocheza na Chelsea Mwaka 2008 huko Moscow na Man United kuibuka Bingwa kwa mikwaju ya penati tano tano.
 Making his point: Robben celebrates scoring from the penalty spot and hauling Bayern level on aggregate
Juzi, Nyota wa Barcelona, Lionel Messi, nae alikosa penati Barcelona walipotolewa na Chelsea kwenye Nusu Fainali nyingine.
Kwenye Fainali ya Mei 19 na Chelsea, Bayern Munich itacheza bila ya David Alaba, Holger Badstuber na Luiz Gustavo kwa kupewa Kadi za Njano kama vile Chelsea watakavyo wakosa Ramires, John Terry, Branislav Ivanovic na Raul Meireles.
 Sacre Bleu: Bayern's French playmaker Franck Ribery reacts after missing a shot on goal
Hii itakuwa mara ya pili kwa Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kuchezwa huku Timu ya nyumbani ikiwemo na mara ya kwanza ilikuwa ni Uwanja wa Santiago Bernabeu wakati Real Madrid ilipoichapa Fiorentina 2-0 Mwaka 1957 na ile ya Lverpool kuifunga AS Roma kwa penati 4-2 baada ya kutoka 1-1 katika Dakika 120 Uwanjani Stadio Olimpico Mwaka 1984.

Football's coming home: Bastian Schweinsteiger celebrates after scoring the final penalty
 Bastian Schweinsteiger ndiye aliyewamaliza Real kwa penati ya mwisho na  kutoka kifua wazi jana

FAINALI
Jumamosi Mei 19
Fußball Arena München [Allianz Arena], Munich, Ujerumani
Bayern Munich v Chelsea

No comments:

Post a Comment