BUKOBA SPORTS

Thursday, April 12, 2012

RONALDO ATIMIZA MABAO 52 MSIMU HUU. YAILAZA ATLETICO 4-1 KWA 'HAT- TRICK'

Ronaldo alifunga hat-trick usiku wa jana



Cristiano Ronaldo ametimiza mabao 52 msimu huu, Real Madrid ikiilaza Atletico mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Vicente Calderon usiku huu.

Mreno huyo alifikisha mabao hayo baada ya kufunga mabao matatu katika dakika za 25, 67 na 82 kwa penalti.


Wakati bao la kufutia machozi la Atletico Madrid lilifungwa na Falcao dakika ya 54, bao lingine la Real lilifungwa na Callejon dakika ya 87.


Katika La Liga pekee, amefunga mabao 40 katika mechi 32.


Ronaldo alifunga mabao 53 katika mechi 54 msimu uliopita, na zikiwa zimebaki mechi sita ligi kuisha msimu huu, ana nafasi ya kuongeza mabao pia kwenye Ligi ya Mabingwa.

Jana, nyota wa Barcelona, Lionel Messi jana ametimiza mabao 61 msimu huu, hivyo kuwa mchezaji wa kwanza katika Ligi kubwa Ulaya tangu mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich, Gerd Muller kufikisha idadi hiyo ya mabao.

No comments:

Post a Comment