BUKOBA SPORTS

Monday, May 14, 2012

AL AHLY SHANDY YASHINDA PENATI 9-8 NA KUITOA MASHINDANONI SIMBA HUKO SUDAN

Yachapwa 3-0, yatolewa kwa Penati 9-8!
Tanzania leo imejikuta haina hata Klabu kwenye michuano ya Afrika baada ya Simba kutandikwa bao 3-0 na Al Ahly Shandy huko Mjini Shandi, Sudan katika Mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho na kufanya Mshindi apatikane kwa tombola ya mikwaju ya penati kwa vile Simba nao waliwachapa Wasudan hao bao 3-0 Mjini Dar es Salaam.
Kwenye hizo penati Al Ahly Shandy walifunga penati 9-8 na kuibwaga nje Simba.
Baada ya kuamriwa kupigwa penati kwa kanuni za mashindano hayo. Timu ya Al Ahly Shandy imeshinda penati 9-8 dhindi timu ya Simba na kuisukumiza nje ya mashindano.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam Simba ilishinda magoli 3-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ili kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrka (CAF) vizuri.

Hata hivyo imeshindwa kulinda ushindi wake mnono ilioupata jijini Dar es salaam na kukubali kipigo hicho kilichowasukumiza nje ya mashindano hayo. 


MECHI ZA MARUDIANO:
MATOKEO:
[Kwenye mabano Matokeo Mechi ya kwanza/Jumla ya Mabao Mechi 2]
Jumamosi Mei 12
Club Africain - Tunisia 4 Royal Leopards – Swaziland  2[5-2]
AS Bamako - Mali 1 Wydad Athletic Club – Morocco 0 [1-3]
Jumapili Mei 13
CODM Meknès - Morocco 0 ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast  0 [1-1]
Alamal Atbara - Sudan 0 GD Interclube – Angola 2 [1-6]
Black Leopards - South Africa 2 Warri Wolves – Nigeria 0 [3-3, Leopards wapita bao]
Cercle de Bamako - Mali 3 Enppi – Egypt  0 [4-3]
Ahli Shandi - Sudan 3 Simba – Tanzania 0 [3-3, Penati 9-8]
AC Leopards de Dolisie - Congo 2 Heartland FC – Nigeria 1 [4-3]

No comments:

Post a Comment