Aston Villa imemtimua Meneja wake Alex McLeish baada ya kushika wadhifa huo kwa Miezi 11 tu na ikiwa ni Siku moja tu baada ya Msimu wa Ligi Kuu England kumalizika.
Msimu huu, Villa imekuwa na wakati mbovu na ilimaliza Ligi ikiwa juu tu ya zile Timu 4 za mwisho na ilishinda Mechi 4 tu za Ligi walizocheza nyumbani Villa Park kati ya jumla ya Mechi 19.
McLeish, mwenye Miaka 53 na Mtu wa Scotland, hakuwa kipenzi cha Mashabiki wa Villa hasa kwa vile alitokea Timu Mahasimu wakubwa Birmingham City.
Uhusiano wake na Mashabiki ulizidi kuzorota kufuatia mwendo mbovu Msimu mzima.
McLeish alichukua Umeneja Villa kutoka kwa Gerard Houllier na kabla aliwahi kuwa Meneja Klabu za Scotland Motherwell na Hibernian na kisha kuhamia Birmingham Novemba 2007 na Timu hiyo kuteremka toka Ligi Kuu lakini Msimu uliofuata, Mwaka 2009, akaipandisha tena Birmingham kurudi Ligi Kuu.
Lakini licha ya kutwaa Carling Cup Februari 2011 kwa kuifunga Arsenal, Msimu huo huo Birmingham ikaporomoka tena Daraja toka Ligi kuu.
REKODI YA McLEISH ASTON VILLA
- Aliteuliwa Umeneja Juni 17, 2011
- Jumla ya Mechi: 42
- Ushindi: 9
- Sare: 17
- Kufungwa: 16
- FA Cup: Walifungwa 3-2 na Arsenal na kutolewa Raundi ya 4
- Carling Cup: Walifungwa 2-0 na Bolton na kutolewa Raundi ya 3
No comments:
Post a Comment