Mayweather (kulia) akiadhibiwa huku damu zikimtoka puani!
LAS VEGAS - MAREKANI BONDIA Floyd Mayweather Jr. ameendeleza ubabe baada ya alfajiri hii kumtandika kwa pointi Miguel Cotto katika pambano lililokuwa kali na la kusisimua.
Mayweather alitumia kasi yake na ufundi kumshinda Cotto, ingawa haikuwa kazi nyepesi kwani mpinzani wake huyo alikuwa akitupa makonde ya maana na kushambulia mwanzo mwisho.
Floyd Mayweather akishangilia baada ya kumpa kichapo Miguel Cotto usiku wa kuamkia leo. ''Wewe ni bingwa hatari,'' Mayweather alimuambia Cotto ulingoni baada ya pambano. 'Wewe ni kinana wa nguvu ambaye sijawhai kukutana naye.''
Mayweather alitawala raundi ya mwisho, ya 12 akimnyanyasa Cotto na kujihakikishia kucheza mapambano 43 bila kupigwa. Tofauti na mapmabano yake mengi, Mayweather alitokwa damu puani mbele ya Cotto.
Majaji wawili walitoa pointi 117-111 na wa tatu akatoa 118-110, hivyo Mayweather ameshinda kwa pointi 116-112. Mayweather aliyepigana wiki chache tu kabla ya kuingia jela ya kutumikia kifungo cha miezi mitatu, alikutana na pambano gumu dhidi ya mplnzani ambaye anakwenda mbele wakati wote.
Akipokea maelezo mafupi Floyd Mayweather jinsi ya kummaliza adui wake Cotto. Lakini alikuwa mwenye kasi na mjanja zaidi ya Cotto na alionekana kumvaa katika raundi za mwisho. Katika raundi ya mwisho, Mayweather alipiga ngumi yake bora zaidi kwenye pambano hilo, uppercut ya mkono wa kushoto ambayo ilimpata na kumuumiza Cotto. Mayweather, aliyeahidiwa kupewa dola za Kimarekani Milioni 32, alilazimika kupigana kila dakika katika raundi 12 za pambano dhidi ya mbabe huyo wa Puerto Rico.
Justin Bieber(mwana musiki) akinyanyua mikanda juu baada ya mpambano.
wadau - Justin Bieber, Rapper Lil Wayne, Mayweather and rapper Curtis '50 Cent' Jackson
Floyd Mayweather akishangilia baada ya kumpa kichapo Miguel Cotto usiku wa kuamkia leo.
Akipokea maelezo mafupi Floyd Mayweather jinsi ya kummaliza adui wake Cotto.
Lakini alikuwa mwenye kasi na mjanja zaidi ya Cotto na alionekana kumvaa katika raundi za mwisho.
Justin Bieber(mwana musiki) akinyanyua mikanda juu baada ya mpambano.
wadau - Justin Bieber, Rapper Lil Wayne, Mayweather and rapper Curtis '50 Cent' Jackson
No comments:
Post a Comment