BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 8, 2012

EUROPA LIGI: FAINALI NI LEO JUMATANO KATI YA ATHLETIC BILBAO V ATLETICO MADRID, MECHI KALI ITAKAYOSISIMUA MASHABIKI! SAA 3:45 USIKU

  Klabu za Spain, Atletico Madrid na Athletic Bilbao, zitakutana kwenye Fainali ya UEFA EUROPA LIGI itakayochezwa huko Mjini Bucharest Nchini Romania Jumatano Mei 9.
 
Timu hizi zina historia ndefu ya kukutana kwenye Fainali za Makombe na mara ya kwanza ilikuwa ni kwenye Fainali ya Copa del Rey ya Mwaka 1921 na Athletic Bilbao kuichapa Atletico Madrid bao 4-1.
 
Lakini, mara ya mwisho kukutana tena ilikuwa Fainali ya Mwaka 1985 ya Kombe hilo hilo na safari hiyo Atletico kuibuka kidedea kwa bao 2-1
Rekodi ya Mechi kati ya Klabu hizi ni Atletico kashinda Mechi 10 dhidi ya 9 za Athletic kati ya Mechi 22 walichocheza kati yao kwa Miaka ya hivi karibuni.

Msimu huu kwenye La Liga, Athletic Bilbao walishinda Mechi yao ya nyumbani bao 3-0 Mwezi Oktoba Mwaka jana huku Straika wao hatari Fernando Llorente akipiga mbili  na Mwezi Machi Atletico walilipa kisasi kwa kuichapa Bilbao bao 2-1 na bao zao zote mbili kufungwa na Straika wao Falcao.
Lakini kwenye Msimamo wa La Liga huku Mechi ikiwa imebaki moja tu, Atletico Madrid wapo nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 53 na Athletic Bilbao wao wapo nafasi ya 10 na wana Pointi 49.
Kwa Ulaya, Atletico wana uzoefu mkubwa kupita Athletic Bilbao kwa kufika Fainali 5 za Klabu Ulaya na kushinda mbili, Mwaka 1961/2 walipoifunga Fiorentina na kutwaa Kombe la Washindi la UEFA na Mwaka 2009/10 walipoifunga Fulham na kunyakua EUROPA LIGI.
Mara pekee Athletic Bilbao kuingia Fainali ya Ulaya ni Mwaka 1977 kwenye UEFA Cup na kubwagwa na Juventus kwa magoli ya ugenini.
Lakini, ukirudi kwao huko Spain Athletic Bilbao wana uzoefu mkubwa wa vinyang’anyiro vya Makombe kwa kufika Fainali za Copa del Rey mara 35, wakifungana na Barcelona, na hapo Mei 25 wapo tena Fainali kucheza na Barcelona.
Pia, Atletic Bilbao wametwaa Vikombe vya nyumbani 23 ukilinganisha na 9 vya Atletico de Madrid.

No comments:

Post a Comment