West Ham jana wameifumua Cardiff City bao 3-0 na kutinga Fainali ya Mechi za Mchujo kuwania nafasi moja kuungana na Reading na Southampton kupanda Daraja na kucheza Ligi Kuu England Msimu ujao.
West Ham, ambao waliichapa Cardiff bao 2-0 katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Mjini Cardiff, leo wakicheza nyumbani Uwanja wa Upton Park walifunga bao zao kupitia Kevin Nolan, Vaz Te na Nicky Maynard.

Kwenye Fainali, itakayochezwa Wembley hapo Mei 19, West Ham watacheza na Mshindi kati ya Birmingham na Blackpool ambazo zitarudiana Jumatano Mei 9 huku Blackpool akiwa mbele baada ya kushinda Mechi ya kwanza 1-0.
VIKOSI:
West Ham: Green, Demel, Tomkins, Reid, Taylor, O'Neil, Noble, Nolan, Collison, Cole, Vaz Te
Akiba: Henderson, McCartney, Maynard, Faubert, Lansbury.
Cardiff: Marshall, McNaughton, Hudson, Turner, Taylor, Lawrence, Gunnarsson, Whittingham, McPhail, Mason, Miller
Akiba: Heaton, Kiss, Cowie, Earnshaw, Blake.
Refa: Mike Dean.
No comments:
Post a Comment