Best of the best: Ryan Giggs (centre) with Alan Shearer (left) and David Gill at the ceremony in London
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, na Mchezaji wake Veterani Ryan Giggs ndio wametwaa Tuzo za Ubora kwa Miaka 20 ya LIGI KUU England kwa kuchaguliwa kuwa Meneja Bora na Mchezaji Bora.
Tuzo hizi zimebuniwa ili kusherehekea Miaka 20 tangu LIGI KUU England ianzishwe.
Ferguson, Miaka 70, ameiongoza Manchester United kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 12 na ni mara hizo 12 ndizo pia Ryan Giggs ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu kama Mchezaji.
LISTI ya TUZO na WASHINDI kwa Ubora kwa MISIMU 20:
MCHEZAJI BORA:
Ryan Giggs
MENEJA BORA:
Sir Alex Ferguson
MSIMU BORA:
2011-12
TIMU BORA:
Arsenal ya Mwaka 2003-04 [haikufungwa Msimu mzima]
MSEMO BORA:
Msemo wa Kevin Keegan ‘Napenda Man United wakifungwa’=Mwaka 1996
GOLI BORA:
Wayne Rooney'-Tiki Taka iliyowaua Manchester City Msimu wa 2011-12
MECHI BORA:
Manchester United 4 Manchester City 3 Msimu wa 2009/10
USHANGILIAJI BORA BAADA YA KUFUNGA GOLI:
Eric Cantona-Mwaka 1996 dhidi ya Sunderland
UOKOAJI BORA WA KIPA:
Craig Gordon (Sunderland) alipookoa shuti la Beki wa Bolton Zat Knight 2010
UFUNGAJI BORA:
Alan Shearer-Goli 260
KIPA AMBAE HAKUFUNGWA BAO HATA MOJA KWA MECHI NYINGI:
David James-Mechi 173
WACHEZAJI WANAOFANYA KIKOSI BORA:
Peter Schmeichel; Gary Neville, Tony Adams, Nemanja Vidic, Ashley Cole; Cristiano Ronaldo, Paul Scholes, Steven Gerrard, Ryan Giggs; Thierry Henry, Alan Shearer
Katika kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora, Giggs amembwaga Mchezaji mwenzake wa Man United Paul Scholes na Wachezaji wawili wa Arsenal Thierry Henry na Dennis Bergkamp.
Ferguson amewashinda Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, Bosi wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho, Meneja wa Tottenham Harry Redknapp na David Moyes wa Everton.
Akiongelea kuhusu Ferguson, Giggs ametamka: ‘Tunafahamiana tangu nina Miaka 13.’
Aliongeza: ‘Alijua Jina langu na Majina ya Wazazi wangu! Alijua kila kitu changu japo kidogo na hilo linaonyesha anajali Watu na linamfanya awe bora na Mtu pekee kabisa! Yeye ndie alienisaidia sana katika maisha yangu ya Soka!
No comments:
Post a Comment