RVP, Miaka 28, anaingia Mwaka wake wa mwisho wa Mkataba wake na Arsenal unaomlipa Mshahara wa Pauni 80,000 kwa Wiki lakini Arsenal wako tayari kumpa nyongeza ya Mkataba wa Miaka minne kwa Mshahara wa Pauni 130,000 kwa Wiki na pia dau la Pauni Milioni 5 akisaini huo Mkataba mpya ili kumzuia asifuate njia ile ile ya Wachezaji wao wengine waliokwenda City ambao ni Emannuel Adebayor, Kolo Toure, Gael Clichy na Sami Nasri.
Mipango ya RVP kuhamia Man City imeongezwa nguvu baada ya Wakala wake Kees Vos kuonekana Uwanja wa Etihad hivi juzi lakini amejitetea kwa kusema: ‘Huwa nakwenda kwenye Mechi nyingi za Ligi Kuu pamoja na za City. Nawaangalia Wachezaji wengi na maisha yangu si Van Persie pekee!’
No comments:
Post a Comment