Straika wa Manchester City Mario Balotelli ametajwa na Kocha wa Italy Cesare Prandelli kwenye Kikosi cha awali cha Wachezaji 32 ambao wataanza mazoezi kwa ajili ya Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, EURO 2012, yatakayochezwa huko Poland na Ukraine kuanzia Juni 8 hadi Julai 1.
Mchezaji huyo mwenye vituko hakuchukuliwa Mwezi Februari kuchezea Italy kwa kile Kocha Cesare Prandelli kudai amevunja maadili ya Timu ya Taifa baada ya kumtimba Scott Parker wa Tottenham kwenye Mechi ya Ligi Kuu England wakati akichezea Klabu yake Man City.
Balotelli, ambae ameichezea Italy mara 7, ni Mchezaji pekee toka Ligi Kuu England kwenye Kikosi hicho cha Wachezaji 32 ambacho kitapunguzwa na kufikia 23 hapo Mei 29 ili kuwasilishwa UEFA.
Mchezaji mwingine ambae yumo kwenye Kikosi hicho ni Mchezaji wa AC Milan Antonio Cassano ambaye Mwaka jana alifanyiwa operesheni ndogo ya moyo na kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi 6 hadi aliporudi tena hivi karibuni.
Pia, Kocha Prandelli amewaita Wachezaji kadhaa kwa mara ya kwanza na hao ni Beki wa Rubin Kazan Salvatore Bocchetti, Straika wa Udinese Antonio Di Natale. Mchezaji kutoka Pescara, Marco Verratti, Kiungo wa Bologna Alessandro Diamanti, Straika wa Siena Mattia Destro, Mchezaji wa Juventus Emanuele Giaccherini na Winga wa Atalanta Ezequiel Schelotto.
Kabla ya kucheza EURO 2012, ambako wako Kundi C pamoja na Spain, Republic of Ireland na Croatia, Italia watajipima nguvu na Luxembourg na Russia.
Kikosi kamili:
Buffon (Juventus), De Sanctis (Napoli), Sirigu (Paris St Germain), Viviano (Palermo); Abate, Astori (Cagliari), Balzaretti (Palermo), Barzagli (Juventus), Bocchetti (Rubin Kazan), Bonucci (Juventus), Chiellini (Juventus), Criscito (Zenit St Petersburg), Maggio (Napoli), Ogbonna (Torino), Ranocchia (Inter Milan); Cigarini (Atalanta), De Rossi (Roma), Diamanti (Bologna), Giaccherini (Juventus), Marchisio (Juventus), Montolivo (Fiorentina), Thiago Motta (Paris St Germain), Nocerino, Pirlo (Juventus), Schelotto (Atalanta), Verratti (Pescara); Balotelli (Manchester City), Borini (Roma), Cassano, Destro (Siena), Di Natale (Udinese), Giovinco (Parma).
No comments:
Post a Comment