BUKOBA SPORTS

Thursday, May 10, 2012

nPOWER CHAMPIONSHIP: WAKUPANDA LIGI KUU ENGLAND NI WEST HAM AU BLACKPOOL!

MCHUJO KUTAFUTA TIMU MOJA KUUNGANA na Reading & Southampton LIGI KUU!!
 Off and running: Blackpool's Stephen Dobbie (left) celebrates scoring his side's opening goal
Blackpool imetoka sare bao 2-2 na Birmingham na kufanikiwa kuingia Fainali ya Mechi za Mchujo kuwania nafasi moja kuungana na Reading na Southampton kupanda Daraja na kucheza Ligi Kuu England Msimu ujao.
 Level pegging: Curtis Davies scores the equaliser for Birmingham against Blackpool
Blackpool, ambao walishinda Mechi ya kwanza nyumbani kwao kwa bao 1-0, Jana usiku  walijikuta wakiongoza bao 2-0 lakini Birmmingham walisawazisha na kuleta mshikemshike uwanjani hapo kwa kuzirudisha goli zote walizokuwa wamefungwa.
 Down: Marlon King and Nikola Zigic (left) stand dejected after conceding their first goal
Blackpool sasa watakutana na West Ham kwenye Fainali itakayochezwa Uwanja wa Wembley ili kupata Timu moja itayoungana na Reading na Southamptom ambazo zimepanda moja kwa moja kwa vile zilimaliza Ligi zikiwa nafasi ya kwanza na ya pili.
Fainali hii ya West Ham na Blackpool itachezwa hapo Mei 19.


FAINALI:
Jumamosi Mei 19
West Ham v Blackpool

No comments:

Post a Comment