Klabu ya Qatar Al Sadd imethibitisha kumsaini Straika Veterani wa Spain Raul kwa ajili ya Msimu ujao. Raul, Miaka 34, alitangaza Mwezi uliopita kuwa ataondoka Klabu ya Bundesliga Schalke mwishoni mwa Msimu huu ingawa amekuwa aking’ara kwenye Timu hiyo tangu ahamie hapo kutoka Real Madrid Mwaka 2010.Al Sadd imefichua usajili huu kwa kutangaza kwenye Tovuti yao na kutamka kuwa Raul ataanuliwa rasmi kwenye Mkutano na Vyombo vya Habari hapo Jumapili Mei 13.
Raul alitangaza rasmi kuihama Schalke Aprili 19 na kusema atachezea nje ya Ulaya lakini hakutaja Klabu gani ila alisema atapenda kuchezea Ligi ambayo sio ngumu kama Bundesliga ili apate muda mwingi kuwa na Familia yake.
Alisema: ‘Naamini naweza kucheza Ligi yeyote ngumu lakini tatizo ni Familia. Bundesliga ni ngumu na nimekuwa sipata muda mwingi wa kuwa na Familia yangu.’
Wachezaji wengine maarufu ambao wapo Al Sadd kwa sasa ni pamoja na Nadir Belhaj na Mamadou Niang.


No comments:
Post a Comment