BUKOBA SPORTS

Monday, May 7, 2012

SERIE A: JUVE BINGWA!

Juventus celebrate scoring against Cagliari - their win sealed the Serie A title
Juventus leo wametwaa Ubingwa wa Italia Serie A baada ya kuwafunga Cagliari bao 2-0 na wapinzani wao waliokuwa wakiwafukuza AC Milan kutandikwa bao 4-2 kwenye Dabi ya Milano na Mahasimu wao Inter Milan.
Juve, ambao walishushwa Daraja Mwaka 2006 na kupokonywa Ubingwa wao wa Miaka ya 2005 na 2006 kwa kuhusishwa na Skandali ya kupanga Mechi matokeo, Msimu huu hawajafungwa hata Mechi moja na wameshinda Mechi 22, sare 15 na wamebakisha Mechi moja tu kumaliza Ligi.Juventus end long wait for Italian title
Bao za Juve za leo zilifungwa na Mirko Vucinic na Marco Borriello.
Huko Milano, Diego Milito alipiga hetitriki, zikiwemo penati mbili, na Maicon kupiga bao moja na kuwapa Inter Milan ushindi wa bao bao 4-2 dhidi ya Mahasimu wao AC Milan ambao bao zao zilifungwa na Zlatan Ibrahimovic.

No comments:

Post a Comment