Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu ipo Khartoum kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Merreikh, hatua ya 16 Bora.
Katika vurugu hizo, basi walilokuwa wamepanda wachezaji wa Mazembe limevunjwa vioo ambapo hali za wachezaji bado hazijajulikana na sasa mechi hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Omdurman, hatima yake ipo mikononi mwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF)- ambalo linatarajiwa kuchukua hatua muda mfupi ujao, kubwa zaidi ikitarajiwa kuifuta mashindanoni Merreikh na kuifungia, hivyo Mazembe kusonga mbele. (kwa mujibu wa shaffihdauda.com)
Simba ambayo nayo iko Sudan kwa ajili ya mechi yao ya jumapili nayo imekiri kufanyiwa vitimbi ikiwemo kuzimiwa taa za uwanja wakiwa mazoezini, kulazwa hosteli badala ya hotelini pamoja na fitina nyingine kibao.
.
No comments:
Post a Comment