BUKOBA SPORTS

Sunday, May 13, 2012

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF, LIMEMTANGAZA KOCHA WA VIJANA KIM POULSEN KUWA KOCHA MPYA WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA (TAIFA STARS)

Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF limemtangaza kocha wa vijana Kim Poulsen kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kuziba nafasi ya aliyekuwa kocha mkuu Jan Poulsen.Rais wa TFF, Leodgar Tenga amesema Kim amepewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Shirikisho kuamua kutomuongezea mkataba Jan Poulsen ambaye Mkataba wake wa miaka miwili unamalizika Julai 30 mwaka huu.
Amesema kwa vile Taifa Stars inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Dunia raundi ya pili Kanda ya Afrika na mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN), TFF imeona ni lazima iwe na kocha mpya mapema kabla ya mkataba wa Jan kumalizika.

Kim amekuwa nchini kwa mwaka mmoja sasa akifundisha timu za Taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na miaka 20 (Ngorongoro Heroes), hivyo anawafahamu vizuri wa wachezaji wa Tanzania.

Naye Kim Poulsen ambapo siku ya Jumatatu Mei 14 atatangaza kikosi cha Taifa Stars ambacho Juni 2 kitaivaa Ivory Coast katika mechi ya mashindano , amesema yuko tayari kwa kazi hiyo na kusisitiza kuwepo ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali ili timu hiyo iweze kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment