Chris Hughton meneja mpaywa Norwich City
Klabu ya Norwich City imemteua meneja wa Birmingham City, Chris Hughton kuwa meneja wake mpya.
Hughton ambaye enzi zake za kusakata kandanda aliwahi kuichezea klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland akicheza nafasi ya ulinzi, alifanikiwa kuifikisha Birmingham katika hatua ya kucheza mechi za mwisho kuwania kupanda ngazi ya Ligi Kuu ya England msimu uliopita ambapo walitolewa na Blackpool.
Norwich hawakuwa na meneja tangu Lambert alipoondika katika klabu hiyo na alitangazwa kushika hatamu za kuinoa Aston Villa tarehe 2 mwezi huu wa Juni.
Kupitia mtandao wa kijamii wa tweeter klabu ya Birmingham iliandika: "Klabu ingependa kumshukuru Chris Hughton na kikosi chake kwa jitahada walizoonesha kwa muda wa miezi 12. Kazi ya kumsaka meneja mpya imeanza."
Norwich City wamemaliza msimu uliopita wakiwa nafasi ya 12 kwenye chati english premiere ligi!
No comments:
Post a Comment