BUKOBA SPORTS

Saturday, June 23, 2012

EURO 2012: GERMANY WAPETA, WASOGEA ROBO FAINALI - KUIVAA ENGLAND AU ITALY!

Katika Mechi ya Robo Fainali ya EURO 2012Germany imeitandika Greece bao 4-2 na kutinga Nusu Fainali.
Baada ya kosa kosa nyingi za Mafowadi wake, katika Dakika ya 39, Nahodha wa Germany Philipp Lahm aliamua kwenda mwenyewe kufunga alipopokea pasi toka kwa Sami Khedira na kuachia mkwaju wa Mita 20 uliotinga wavuni na kumwacha Kipa wa Greece, Sifakis, akiruka bila mafanikio.
Kipindi cha Pili, kaunta ataki safi ya Greece ilimkuta Giorgos Samaras aliemalizia vizuri na kuifanya gemu iwe bao 1-1.
Lakini Germany walicharuka na kuchapa bao 3 kupitia Sami Khedira, Dakika ya 61, Miroslav Klose, Dakika ya 68 na Reus, Dakika ya 74.
Greece walipata bao la pili kwa penati ya Salpingidis ya Dakika ya 88 baada ya Jerome Boateng kuunawa mpira.
Kwenye Nusu Fainali, Germany watacheza na Mshindi wa Mechi ya Robo Fainali itakayochezwa Jumapili kati ya England na Italy.
VIKOSI
Germany (4-2-3-1): Neuer; Boateng, Hummels, Badstuber, Lahm; Khedira, Schweinsteiger; Reus, Ozil, Schurrle; Klose.
Akiba: Wiese, Gundogan, Schmelzer, Howedes, Podolski, Muller, Bender, Mertesacker, Kroos, Gotze, Gomez, Zieler.
Greece (4-2-3-1): Sifakis; Torosidis, Papastathopoulos, Kyriakos Papadopoulos, Tzavellas; Makos, Maniatis; Ninis, Katsouranis, Samaras; Salpingidis.
Akiba: Chalkias, Malezas, Liberopoulos, Mitroglou, Fotakis, Gekas, Fortounis, Fetfatzidis, Tzorvas.
Refa: Damir Skomina (Slovenia)
RATIBA/MATOKEO
ROBO FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Alhamisi Juni 21
RF1: Warsaw, Poland: Czech Republic 0 Portugal 1
Ijumaa Juni 22
RF2: Gdansk, Poland: Germany 4 Greece 2
Jumamosi Juni 23
RF3: Donetsk, Ukraine: Spain v France
Jumapili Juni 24
RF4: Kiev, Ukraine: England v Italy
NUSU FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Jumatano Juni 27
NF1: Donetsk, Ukraine: Portugal v Spain/France
Alhamisi Juni 28
NF2: Warsaw, Poland: Germany v England/Italy
FAINALI
Jumapili Julai 1
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Kiev, Ukraine: NF1 v NF2

No comments:

Post a Comment