BUKOBA SPORTS

Friday, June 22, 2012

EURO 2012: RONALDO AIPELEKA PORTUGAL NUSU FAINALI, KUCHEZA NA SPAIN AU FRANCE!

Nahodha wa Portugal, Cristiano Ronaldo, jana ameibeba Nchi yake Portugal kwa kufunga bao moja na la ushindi dhidi ya Czech Republic kwenye Mechi ya Robo Fainali ya EURO 2012.
Katika Mechi iliyokuwa ya upande mmoja kwa muda mwingi huku Portugal wakitawala na kukosa bao kadhaa zikiwemo mbili za Ronaldo ambazo ziligonga posti, iliwachukua Portugal hadi Dakika ya 79 kupata bao lao la ushindi kufuatia krosi ya Moutinho toka kulia kuunganishwa kwa kichwa cha Ronaldo kilichodunda chini na kumpita Kipa Petr Cesc.
Kwenye Nusu Fainali, Portugal watacheza na Mshindi kati ya Spain na France.Ronaldo alijaribu sana lakini dakika 79 aliweza kufunga, baada ya kosa kosa nyingi kutokea!

Wakiangalia mtanange kwa makini Portuguese luminaries Eusebio na Figo ndani ya Warsaw
VIKOSI
Czech Republic: Cech; Gebre Selassie, Sivok, Kadlec, Limbersky; Hubshman, Plasil; Jiracek, Darida, Pilar; Baros
Portugal: Patricio; Pereira, Pepe, Alves, Coentrao; Meireles, Veloso, Moutinho; Nani, Postiga, Ronaldo
Refa: Howard Webb [England]
RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Alhamisi Juni 21
RF1: Warsaw, Poland: Czech Republic 0 Portugal 1
Ijumaa Juni 22
RF2: Gdansk, Poland: Germany v Greece
Jumamosi Juni 23
RF3: Donetsk, Ukraine: Spain v France
Jumapili Juni 24
RF4: Kiev, Ukraine: England v Italy
NUSU FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Jumatano Juni 27
NF1: Donetsk, Ukraine: Portugal v Spain/France
Alhamisi Juni 28
NF2: Warsaw, Poland: Germany/Greece v England/Italy
FAINALI
Jumapili Julai 1
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Kiev, Ukraine: NF1 v NF2

No comments:

Post a Comment