BUKOBA SPORTS

Friday, June 22, 2012

CLARENCE SEEDORF NA YEYE AAGA MILAN!

SEEDORF aungana na WAKONGWE Gattuso, Nesta, Inzaghi, Zambrotta & Van Bommel kung’atuka!
AC Milan, ambayo iko mbioni kujiimarisha upya, imechukua Wachezaji wawili wapya baada ya kutangazwa rasmi Clarence Seedorf kaamua kuachia ngazi baada ya utumishi wa Miaka 10 na kuwafuata Wakongwe Gennaro Gattuso, Alessandro Nesta, Filippo Inzaghi, Gianluca Zambrotta na Mark van Bommel ambao wote wameondoka mara Msimu huu ulipomalizika.
Katika kujiimarisha AC Milan imeshakubaliani kuwasaini Beki wa Chievo Francesco Acerbi na Kiungo kutoka Guinea anaechezea Genoa, Kevin Constant.
Hadi sasa haijajulikana Seedorf anaelekea wapi ingawa zipo habari kuwa pengine huenda kucheza Brazil katika Klabu ya Botafogo.
Mwenyewe Seedorf, mwenye Miaka 36, amesema amepata ofa nyingi lakini ataamua baadaye.
Mchezaji mwingine wa AC Milan ambaye ameachwa ni Kiungo wa zamani wa Arsenal Mathieu Flamini.
Inter Milan, chini ya Kocha Massimiliano Allegri, tayari imeshawachukua Mchezaji wa Fiorentina Riccardo Montolivo na yule wa Nancy ya Ufaransa Bakaye Traore.

No comments:

Post a Comment