Borini, Miaka 21, ambaye sasa yuko na Timu ya Taifa ya Italy kwenye Fainali za EURO 2012, si mgeni kwa Meneja mpya wa Liverpool Brendan Rodgers ambaye aliwahi kumfundisha Borini wote walipokuwa pamoja Chelsea huku Rodgers akiwa ndie Kocha wa Timu ya Vijana.
Pia, Rodgers wakati akiwa Swansea City, alimchukua Borini kwa mkopo na Mchezaji huyo akawafungia bao 6 katika Mechi 9.
Msimu uliopita, Borini alikuwa AS Roma kwa mkopo na kufunga bao 9 katika Mechi 24.
No comments:
Post a Comment