Kutokana na matokeo hayo, Uholanzi ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo imeondolewa ikiwa haina pointi hata moja.
Ronaldo ambaye hakufanikiwa kuonyesha kiwango kizuri kwenye michezo miwili ya awali dhidi ya Denmark na Ujerumani, alianza kwa kuisawazishia Ureno katika dakika ya 27, akifuta bao la dakika ya 11 lililofungwa na Rafael Van De Vaart.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alipambana zaidi na kufunga bao safi katika dakika ya 74 ya mchezo baada ya kuwapiga chenga mabeki wawili wa Uholanzi.
Katika mchezo mwingine, Ujerumani ilifanikiwa kuiangamiza Denmark na kumaliza kundi hilo bila kufungwa, shukrani kwa mabao yaliyofungwa na Lukas Podolski katika dakika ya 19 na Lars Bender.
Denmark ilijipatia bao lake kupitia kwa Michael Krohn-Dehli. Ujerumani na Ureno ndiyo zimefanikiwa kuingia kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi kwa Bara la Ulaya.
ROBO FAINALI: Germany v Greece & Portugal v Czech Republic
Kwenye Mechi za mwisho za Kundi B la Fainali za EURO 2012, Portugal walitoka nyuma kwa bao 1-0 walipotanguliwa na Netherlands kwa bao la Dakika ya 11 la Rafael van der Vaart na kushinda bao 2-1 huku bao zote zikifungwa na Cristiano Ronaldo katika Dakika za 28 na 74.
Ushindi huo umewafanya Portugal waingie Robo Fainali wakiwa nafasi ya pili, nyuma ya Germany, na kwenye Robo Fainali watacheza na Czech Republic, waliotwaa nafasi ya kwanza ya Kundi A, Mechi ambayo itachezwa Alhamisi Juni 21.
Nao Germany wamefanikiwa kushinda Mechi ya 3 mfululizo kwenye Kundi B walipoifunga Denmark bao 2-1 kwa bao za Lukas Podolski, Dakika ya 19, na Lars Bender, Dakika ya 80.
Bao la Denmark lilifungwa na Michael Krohn-Dehl katika Dakika ya 24.

Germany watacheza na Greece, waliomaliza nafasi ya pili toka Kundi A, kwenye Robo Fainali itakayochezwa hapo Ijumaa Juni 22.
Germany wakishangilia goli la Bender
MSIMAMO KUNDI B
| NCHI | P | W | D | L | GD | PTS |
| GERMANY | 3 | 3 | 0 | 0 | 3 | 9 |
| PORTUGAL | 3 | 2 | 0 | 1 | 1 | 6 |
| DENMARK | 3 | 1 | 0 | 2 | 1 | 3 |
| NETHERLANDS | 3 | 0 | 0 | 3 | -3 | 0 |
RATIBA:
Jumatatu, Juni 18
KUNDI C
Saa 3 Dak 45 Usiku
Gdansk, Poland
Croatia v Spain
Poznan, Poland
Italy v Republic of Ireland
-------------------------
Jumanne, Juni 19
KUNDI D
Saa 3 Dak 45 Usiku
Donetsk, Ukraine
England v Ukraine
France v Sweden
ROBO FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Alhamisi Juni 21
RF1: Warsaw, Poland: Czech Republic v Portugal
Ijumaa Juni 22
RF2: Gdansk, Poland: Germany v Greece
Jumamosi Juni 23
RF3: Donetsk, Ukraine: Mshindi C v Mshindi wa Pili D
Jumapili Juni 24
RF4: Kiev, Ukraine: Mshindi D v Mshindi wa Pili C
NUSU FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Jumatano Juni 27
NF1: Donetsk, Ukraine: RF1 v RF3
Alhamisi Juni 28
NF2: Warsaw, Poland: RF2 v RF4
FAINALI
Jumapili Julai 1
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Kiev, Ukraine: NF1 v NF2
No comments:
Post a Comment