Nahodha wa sasa wa England ni Steven Gerrard ambae pia ni Nahodha wa Klabu ya Liverpool.
Rooney, Straika wa Manchester United, atarudi dimban Jumanne kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi D la Fainali za EURO 2012 dhidi ya Wenyeji Ukraine itakayochezwa Donbass Arena Mjini Donetsk huko Ukraine ikiwa ni Mechi yake ya kwanza kwenye Fainali za EURO 2012 baada ya kutumikia Kifungo cha Mechi mbili.
Kwenye Mechi hiyo na Ukraine, England wanahitaji sare tu ili kutinga Robo Fainali na inategemewa Rooney ataanza Mechi hiyo akiwa patna wa Straika mwenzake wa Manchester United Danny Welbeck.
Akigusia uteuzi wa Makamu wa Nahodha Hodgson alisema: “Hatujachagua Mtu lakini yeye anastahili!”
Nae Rooney ametamka kuwa hali kwenye Kambi ya England ni shwari na inaonekana kama Kambi ya Klabu na si Timu ya Taifa kwa jinsi Wachezaji wanavyopatana na kushirikiana.
Alisema: “Kila Mtu anapatana na mwenzake na tunaaminiana Wachezaji na Viongozi na kila Mtu ana furaha!”
Rooney, Miaka 26, aliongeza: “Tunahisi kama ni Klabu badala ya Timu ya Taifa! Nenda Hotelini uone! Utakuta Wachezaji wa City wanacheza Snuka [aina ya Pool] na Wachezaji wa Man United, Chelsea wanacheza na Liverpool! Kila Mtu anajichanganya, wanaelewana na ni furaha tu!”
No comments:
Post a Comment