TANZANIA kuwa na Klabu 4: Yanga, Simba, Azam & Mafunzo!
Kuna taarifa kuwa Klabu ambazo si Wanachama wa CECAFA [Council of East and Central African Football Associations] Baraza la Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki na Kati, hazitaalikwa kushiriki Mashindano ya kutafuta Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup, baada ya Klabu 12 toka Nchi Wanachama kuthibitisha ushiriki wao na kuzibakisha Klabu mbili tu, Red Sea FC (Eritrea) na El Merreikh (Sudan), kuwa ndio ambazo bado kutoa uthibitisho wa ushiriki wao.
KLABU ambazo tayari zimethibitisha kushiriki ni Yanga, Azam FC, Simba SC (Tanzania Bara), Mafunzo (Zanzibar), Tusker (Kenya), URA (Uganda), APR (Rwanda), Atletico (Burundi), Elman (Somalia), Ports (Djibouti), Wau Salam (South Sudan) na Coffee (Ethiopia).
Kagame Cup itachezwa Dar es Salaam kuanzia Julai 14 hadi 29.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, Klabu ambazo hazitoki Nchi Wanachama zilizoomba kucheza Kombe hili kama Wageni waalikwa ni Vita Club (Congo DR), Bloemfontein Celtics, Platinum FC, Silver Stars FC (South Africa) na Dynamos (Zimbabwe).
Yanga ndiyo Mabingwa Watetezi wa Kagame Cup baada ya kuifunga Simba bao 1-0 kwenye Fainali ya Mwaka jana iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa bao la Straika kutoka Ghana Kenneth Asamoah.
No comments:
Post a Comment