Timu hizo 4 ndio zimebaki kuwania kutwaa Kombe liitwalo Henri Delaunay ambalo litaanikwa Uwanjani Stadion NSK Olimpiyskiy Mjini Kiev Nchini Ukraine hapo Jumapili Julai 1.
Mabingwa Watetezi Spain, ambao pia ni Mabingwa wa Dunia, wanawania kuwa Timu ya kwanza kushinda mfululizo Mashindano makubwa matatu baada ya kutwaa EURO 2008 na Kombe la Dunia Mwaka 2010.
Pia, Spain wakifanikiwa kulitetea Taji lao la EURO watakuwa Nchi ya kwanza kuweza kutwaa Ubingwa wa Ulaya mara mbili mfululizo.
SPAIN v PORTUGAL
Lakini Spain kwanza lazima wasake ushindi ndani ya Donbass Arena dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Portugal kama walivyofanya kwenye Raundi ya Timu 16 ya Kombe la Dunia mwaka 2010 huko Afrika Kusini wakati bao la Kipindi cha Pili la David Villa lilipowapa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Portugal.
Kwenye Mashindano ya EURO, mara ya mwisho kwa Spain na Portugal kukutana ilikuwa ni kwenye EURO 2004 iliyochezwa huko Ureno na Nuno Gomes kuwapa Portugal ushindi wa bao 1-0 ambao uliwatupa nje Spain.
Mara ya mwisho kwa Nchi hizi kucheza ilikuwa kwenye Mechi ya kirafiki huko Lisbon Mwezi Novemba 2010 na Portugal ikaibomoa Spain kwa bao 4-0.
Kwa sasa kwenye EURO 2012, Kikosi cha Kocha Paulo Bento kinapeta vizuri huku Staa wao Cristiano Ronaldo akiwaka kwa kuwafungia bao zao zote katika Mechi zao mbili zilizopita walipowafunga Netherlands 2-1 na Czech Republic bao 1-0.
Lakini Spain wapo kwenye morali nzuri baada ya kuifumua Timu iliyokuwa ikisifiwa sana France bao 2-0 kwenye Robo Fainali.
GERMANY v ITALY
Siku inayofuata, Alhamisi, Italy watavaana na Germany hii ikiwa ni mara ya kwanza kukutana katika Mashindano rasmi tangu Mwaka 2006 Germany walipotolewa na Italy kwenye Nusu Fainali za Kombe la Dunia.
Katika Mechi 30 walizokutana, Italy wameshinda mara 14, Germany mara 9 na sare 7.
Germany haijaifunga Italy kwenye EURO na Kombe la Dunia na wameshakutana mara 7 kwenye Mashindano hayo huku Italy wakishinda mara 3 na sare 4.
Lakini Kikosi cha sasa cha Germany chini ya Kocha Joachim Low ni moto wa kuotea mbali na kwenye hii EURO 2012 ndio Timu pekee ambayo imeshinda Mechi zake zote 4 hadi sasa na pia ndio Timu iliyofunga bao nyingi.
RATIBA
NUSU FAINALI=[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Jumatano Juni 27
Donetsk, Ukraine=Donbass Arena
Portugal v Spain
Alhamisi Juni 28
Warsaw, Poland=Stadion NSK Olimpiyskiy
Germany v Italy
FAINALI
Jumapili Julai 1
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Kiev, Ukraine= Stadion NSK Olimpiyskiy
Portugal/Spain v German/Italy
No comments:
Post a Comment