BUKOBA SPORTS

Monday, June 25, 2012

MADAKTARI: NEMANJA VIDIC YUPO FITI SASA !!

VIDIC ambaye aliumia goti Mwezi Desemba wakati Man United wanacheza na FC Basel kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, amepona na kuna mipango kwa yeye kuripoti Wiki moja mapema kabla Wachezaji wenzake kurudi Old Trafford mwanzoni mwa Julai kwa ajili ya Msimu mpya ili kumjenga zaidi.  Madaktari wa Man United wamefurahishwa na maendeleo ya Vidic na wametayarisha programu maalum kwa ajili yake ili awe fiti zaidi na kuweza kuichezea Man United kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Msimu mpya wa 2012/13 hapo Agosti 18 dhidi ya Everton.
TUJIKUMBUSHE KATIKA PICHA
Chicharito na yeye ilimuuma sana...Siku ambayo Nemanja vidic alipoumia, Kocha wake Ferguson alivyoumia na yeye

No comments:

Post a Comment